Assalam Aleykum Waislam wote duniani.Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo sina budi kumtakia rehma na amani Mtume Muhammad s.a.w. , Watukufu waislamu duniani kote nawatakia kila la heri katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mwezi wa Ramadhan ni moja ya nguzo za Uislamu,Kwa kila mmoja mwenye afya kamili bila maradhi ameamrishwa kufanya Ibada ya Funga,hivyo nawakumbishia kila mmoja mwenye umri ambao kisheria anatakiwa kufunga hana budi kufanya hivyo.
Nawaombea Dua kila mmoja aweze kufanya Ibada hiyo ya funga,Mungu amuepushe na vishawishi vitakavyoibatilisha funga yake Ameen.Funga ni ngumu ila ina wepesi mkubwa sana kwa mwenye nia ya ukweli katika kuifunga.Nawatakia kila la heri kwa kila mmoja atakayejaaliwa kufunga.