Kuna taifa la Uchina,yani hawa jamaa kila nchi utakayobahatika kufika utakutana nao wamewekeza sio mchezo.Nilipokuwa nazungukazunguka mitaani nilikutana na baadhi ya mitaa ni maduka yao tu,na kwa kukuhakikishia kuwa maeneo hayo wapo wao tu basi hufanya jitihada za ziada kununua mtaa na kuupa jina la nchi yao.Angalia alama waliyoiweka juu hapo,yani utajua tu kwamba hapa wachina wapo.
 Kama na sisi pale Ubungo bus terminal pangekuwa hivii yani ingependeza sana.Kila bus lipo kwenye mstari wake na litaondoka kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopangwa na serikali na sio watu kujiamulia hovyo.Angalia usafi wa barabara zao hakuna hata kipande cha karatasi,sio kwetu maganda ya ndizi,maganda ya machungwa na uchafu unaozagaa hovyo.
Nilivutiwa sana na kituo hiki cha bus,Kipo Holland na kinajulikana kama Holland Spoor ama kwa kifupi HS.mabasi masafi njia safi na watu wake pia wasafi.
 Ukiingia ndani ya bus unaweza kulipa cash au unalipia kwa Card maalumu kama unavyoniona hapo pichani niki`scan card maalumu kama ishara ya kulipia nauli ya bus na trip ninayokwenda.madereva wao wapo makini sana,huwezi kupanda bus bila kulipa nauli na wana huduma nzuri na kauli zao pia ni nzuri kwa wateja tofauti na baadhi ya makondakta na madereva wa kwetu.bus hili halina kondakta ni dereva tu anamalizana na wewe kwa kila kitu.
Serikali ndio yenye wajibu wote wa kuhakikisha mazingira ya nchi yanakuwa safi,hapa unaweza kuona wafanyakazi wa serikali wakifanya usafi kwenye baadhi ya nyumba za wakazi.kiukweli nchi za wenzetu wanajitahdi sana juu ya usafi wa mazingira ya wananchi wao.na hili nahisi kiukweli hata sisi kwetu linawezekana.
 Kwa mtaji huu huwezi kupata mazalio ya mbu kamwe.Ulaya baadhi ya nchi kuna mbu ila mbu wake hawana maradhi.
 Pichani kama unavyojionea,mwananchi kaweka mapipa maalumu ya plastic yenye uchafu,halafu wafanyakazi wa serikali wanayapitia kwa magari maalumu ya kuzoa uchafu,nakumbuka hata sisi magari haya yalishawahi kuletwa ila wananchi waliyaharibu kwa kuingiza vyuma  ndani ya magari hayo.
 Ebu ona jinsi gari la kuzolea uchafu lilivyo safi na mfanyakazi wake,angalia barabara ilivyosafi na alama zake ,kiukweli tunahitaji jitihada za lazima ili tuwe kama wenzetu.
 Hiki ni kifaa maalumu cha kudhibiti mwendo barabarani,ukizidisha mwendo unaonywa kwa alarm ndani ya gari yako,ukiendelea kuzidisha mwendo kuna camera maalumu ambazo zimefichwa kwenye nguzo barabarani humo zinapiga picha namba ya gari lako kisha unaletewa bill kama adhabu na uenda ukapelekwa mahakamani au kufungwa kabisaa.
Hii round about ilinikumbusha sana pale shule ya uhuru Kariakoo,yani na yetu ingekuwa hivii tungekuwa tunachekea tumboni.
 Wenzetu bwana...!!!!! unajua hapa nilikuwa nafanya nini? nimesimama kituoni naangalia muda wa bus langu litakuja saa ngapi na dakika ngapi zimebaki ili lije.Mabasi ya wenzetu yanakuja kituoni kwa muda maalumu na sio mabasi kujazana kituoni,kila nbasi linakuja kwa muda uliopangwa.kila la heri serikali yangu kwa kweli najifunza mengi sana nchi za watu.Nami nikipewa Ubunge nita.............
Pale kituoni nilipokuwa naangalia muda wa bus,hiki ndio kifaa nilichokuwa nakianagalia,kushoto kinanionyesha bus namba na kulia muda wa bus litakavyoondoka,yani kinakuonyesha muda wa bus litakavyoondoka na zimebaki dakika ngapi ili bus lifike,Duuuh kweli tembea ujionee...kwetu yaani ni full msaada kwenye tuta.
 Nilibahatika kutembelea hospital kubwa sana jijini LEIDEN,na kuna baadhi ya mgonjwa ambaye alilazwa pale ni mtoto wa shemeji yangu Aziz pichani kushoto.Nilimuona mtoto wa shemeji Aziz aliyelazwa hospitalini hapo,hali yake ilikuwa nzuri japo alikuwa bado yupo chini matibabu.Maganga One Blog inamtakiwa afya njema na kupona kwa haraka kwa mtoto wa shemeji.Hospitalini hapo kiukweli huwezi kujua kama ni hospital au ni nyumbani,maana hakuna hata harufu ya madawa,ni kusafi kupita maelezo na huduma zao sina cha kusema,wanahitaji kila pongezi.
Matembezi yangu yote na safari nzima ya Uholanzi yamefadhiliwa na mwenyeji wangu Shekh Hija,ni huyo hapo pichani juu mwenye kofia nyeusi na sweta la mistarimistari akielekea kunikatia tiketi kwenye kifaa/mashine maalumu ya tiketi ilee mbele ya njano.Kiukweli nilitembezwa sana mpaka nikaomba nisitishe ziara yangu maana sehemu zilikuwa bado ni nyingi sana,Nilifurahi sana kuonyeshwa maeneo mbalimbali na kujifunza mengi sana toka kwa mwenyeji wangu.
Kila lenye mwanzo huwa na mwisho,ziara yangu ilibidi niisitishe kutokana na majukumu mengine ya kulisukuma gurudumu la maisha,nilifungasha virago na kusindikizwa stesheni ya trein kuelekea Nzegaaaaaaaa.Kushoto ni Shekh Hija ambaye ni mwenyeji wangu nchi Holland,kati ni bwana Jimmy pia ni mwenyeji wangu nchi Holland.
Swahiba wangu Jimmy kushoto ambaye hivi karibuni kavuta jiko hakubaki nyuma katika kunipa kampani mpaka kituo cha reli,maana nilikuwa na vijizawadi kedekede kwenye vijibegi vyangu.
Reli ya kati kigoma ilikuwa na matengenezo ikawa kila tukifika sehemu tunabadilisha trein,ila mambo yalikwenda sawa na MUNGU alinijaalia kufika salama Nzega.kiufupi safari yangu ya Holland niliinjoi sana na kujifunza mengi ila nikaonelea nigawane nanyi machache,mwenye maoni Ruksaaaaa........yangu ni hayo tu.