Kila raia alihofia usalama wake na kufanya baadhi ya watu kukimbia hovyo njiani.
| Sio tu magari yaliyochomwa moto,hata baadhi ya barabara zilifungwa kwa kuchomwa moto matairi ya gari. |
| Kila mmoja aakiwa ameshikwa na bumbuwazi na uwoga juu kwa kuhofia nini kitafuata,kwa kweli timbwili hili la wanachinga lilitikisa jiji la Mwanza hapo jana.(Picha zote na Ibrahim Maganga toka Mwanza) |
JIJI la Mwanza jana liligeuka uwanja wa vita kutokana na vurugu za wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga, waliovamia maduka, kuchoma magari na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa.
Wafanyabiashara hao wanadaiwa kufanya vurugu hizo kushinikiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji hilo kuwaruhusu waendelee kufanya biashara katika maeneo ya katikati.
Wafanyabiashara hao wanadaiwa kufanya vurugu hizo kushinikiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji hilo kuwaruhusu waendelee kufanya biashara katika maeneo ya katikati.
| Wananchi wanapochanganyikiwa huwa hawana hofu na kitu chochote,angalia hii picha. |
Vurugu hizo zilianza saa 2.48 asubuhi katika maeneo ya Sahara, Miti Mirefu na Makoroboi, baada ya mgambo wa Jiji kufika maeneo hayo kuzuia wasifanye biashara.
Mgambo waliwataka waende kwenye maeneo waliyopangiwa kufanyia biashara zao.
Hata hivyo, Wamachinga hao waliwatimua wanamgambo kwa mawe na kushindwa kuwadhibiti. Askari hao walikwenda kujipanga upya na kurudi wakiwa na askari wa Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Mgambo waliwataka waende kwenye maeneo waliyopangiwa kufanyia biashara zao.
Hata hivyo, Wamachinga hao waliwatimua wanamgambo kwa mawe na kushindwa kuwadhibiti. Askari hao walikwenda kujipanga upya na kurudi wakiwa na askari wa Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Baada ya kikosi hicho kuwasili eneo la tukio, Wamachinga waliwarushia mawe na kuchoma matairi katika barabara ya Nyerere karibu na Msikiti wa Ijumaa na kusababisha huduma kwa wananchi na biashara kusimama kwa takribani saa tano.
Gazeti hili lilishuhudia matairi yakiwaka katikati ya barabara, huku kundi la vijana likitoa lugha za kejeli.
Vijana hao walijikusanya na kuvamia kituo cha mafuta cha Moil ingawa hawakufika kutokana na kamba maalumu ilizozungushiwa.
“Mpaka leo kieleweke, lazima kieleweke,” walisikika Wamachinga hao waliokuwa wameshikilia magaloni ya plastiki huku wakinyunyuzia mafuta kwenye matairi na kuyawasha na kufanya baadhi ya watu waliokuwa na magari kurudi maeneo ya katikati ya Jiji na uwanja wa ndege na maeneo ya Isamilo.
Ilipofika saa 6.15 mchana, vurugu hizo zilipamba moto, na Wamachinga hao kuvamia maduka ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia na kupora vitu yakiwamo majokofu, redio na vyombo vya ndani na kuteketeza magari zaidi ya matatu na mengine tisa kupondwa mawe.
Aidha, katika maeneo ya karibu na shule za sekondari za Pamba na Mwanza, walionekana watu wengi wakishuka kwenye daladala na kukimbilia katika shule hizo kwa lengo la kukwepa vurugu hizo.
Jengo ambalo zimo ofisi za Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) inayomiliki magazeti ya HABARILEO na DAILYNEWS ni miongoni mwa yaliyovamiwa na kuvunja vioo kadhaa vya mbele ingawa hakuna kilichoporwa.
Gazeti hili lilishuhudia gari namba T125 AJF na T 196 AKP yakiteketezwa kwa moto. Pia walivamia maduka ya Dubai Bazaar na kuvunja vioo na duka la Zara Solar Ltd likivunjwa na kupora mali na fedha taslimu.
Wamachinga hao walivamia mtaa wa Rufiji katika baa ya Florida na kupora vitu na kuhamia katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure, na kuvunja gari namba T 224 AXC lililokuwa nje na kisha kuharibu jenereta.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Simon Sirro, alisema jana kuwa watu 25 wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, huku wakiwa na baadhi ya vitu walivyopora kwenye tukio hilo.
“Kwa sasa tumekamata watu 25 ambao tumewakuta na vitu walivyopora kwenye maduka na operesheni hii inaendelea, ili kuhakikisha kuwa Jiji la Mwanza linarudia hali ya kawaida, na hawa tuliowakamata tutawafikisha mahakamani mara moja,” alisema na kuongeza kuwa katika tukio hilo, magari mawili yalichomwa moto na kuteketea na mengine tisa kuvunjwa vioo kwa kupondwa mawe.
Hata hivyo, Kamanda Sirro aliagiza askari wake waondoke kwa sababu walifuatwa kuzuia Wamachinga kufanya biashara katika mtaa wa Makoroboi ambako ni maeneo yasiyoruhusiwa, lakini kauli nyingine ikatoka ikiwataka Wamachinga waendelee.
“Hatuwezi kufanya kazi katika migongano, ndiyo maana nimeamuru askari wangu warudi ili kutoa nafasi kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji kukubaliana juu suala hilo la Wamachinga,” alisema Sirro.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, alilaani vurugu hizo, akisema Serikali haitatengua uamuzi wake wa awali wa Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe, kuwataka Wamachinga kuhamia maeneo waliyotengewa kwa biashara zao.
“Nalaani sana hatua hii ya Wamachinga kuendelea kufanya vurugu, nataka watambue, kuwa shughuli zozote zile za kiuchumi katika majiji yoyote duniani zina utaratibu wake, uongozi wa Jiji ulishawatengea maeneo ya biashara kule Kiloleni, na tunawaomba tena warejee kwenye maeneo waliyopangiwa,” alisema.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Francis Mkabenga, alisema operesheni ya kuhamisha Wamachinga kutoka Makoroboi, Miti Mirefu na Mjini Kati, ilianza vizuri, lakini alishangaa kuona baadaye hali ikibadilika.
Wakati baadhi wamelazwa katika Hospitali ya Sekou Toure, wengine walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.
Waliojeruhiwa katika vurugu hizo na ambao wamelazwa Sekou Toure ni Kelvin Jeremia (16) aliyechomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni na kutokea kifuani.
Jeremia alikutwa na dhahama hiyo wakati akienda sokoni. Mwingine ni Omary Abdallah (25) ambaye ni fundi makoroboi aliyejeruhiwa mkono wa kulia.
Mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema majeruhi wengine wawili walikimbizwa Bugando kwa matibabu kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Juma aliyekuwa mahututi kutokana na kujeruhiwa mdomoni na kichwani na Pastory Briton (25) aliyejeruhiwa kwa risasi kiunoni.
Hata hivyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure, Onesmo Rwakyendela, hakupatikana kuzungumzia hali halisi ya wagonjwa waliofikishwa hospitalini hapo kutokana na kuwa katika chumba cha upasuaji.
Mohamed Papia ni mmoja wa wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia ambaye ni mmiliki wa duka la Zara, ambaye alisema baada ya Wamachinga kuvunja vioo na kuingia ndani walipora vitu mbalimbali vikiwamo sola, televisheni, betri, mashine za kuchimbia visima, mashine ya Mamlaka ya Mapato (TRA) pamoja na fedha taslimu ambazo kiasi chake bado hakijajulikana.
“Tunamshukuru Mungu mimi na wafanyakazi wangu hatujadhurika zaidi ya kuporwa mali, tulishindwa kujihami baada ya kundi la watu 50 kuingia ndani kwa pamoja na kila mmoja akibeba alichoweza,” alisema Papia.
(Habari Leo).
0 Comments