Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati mbele) akiwa na wanafunzi wa shule za sekondari waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita baada ya kuwakabidhi vyeti na kuwatambulisha kwa wabunge mjini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Mkuchika na kushoto kwake ni Waziri wa Elimu, Utamaduni na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).