Baba na binti yake ambao walikuwa kwenye penzi zito kwa kipindi cha miaka mitatu, wametupwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kuingia kwenye uhusiano kinyume na maadili ya jamiiAndrew Butler mwenye umri wa miaka 47 ambaye alikuwa akila uroda na binti yake Nicola Yates mwenye umri wa miaka 26, amehukumiwa kwenda jela miezi 10.
Mahakama ya mjini Birmingham ilimuona Andrew na binti yake Nicola wote wana hatia ya kuingia kwenye uhusiano huo haramu uliodumu kwa miaka mitatu wakiishi pamoja kama mtu na hawara yake.
Andrew aliachana na mama yake Nicola mwaka 1992 wakati huo Nicola akiwa na umri wa miaka sita.
Alipokuwa na umri wa miaka 20 Nicola alianza kumtafuta baba yake kwa kutumia mtandao wa rekodi za familia nchini Uingereza unaoitwa Genes Reunited.
Baada ya kufanikiwa kumpata baba yake, Nicola alikuwa karibu zaidi na baba yake na haukupita muda mrefu ukaribu huo uligeuka uhusiano haramu wa kimapenzi kati ya baba na binti yake.
Hii ilikuwa ni mara ya pili wawili hawa kufikishwa mahakamani kwa kosa kama hili.
Mara ya kwanza walinaswa wakiwa na uhusiano huu haramu miaka minne iliyopita ambapo Andrew alihukumiwa kwenda jela miezi minne wakati Nicola alihukumiwa kufanya kazi ngumu za kuitumikia jamii kwa jumla ya miezi 18.
Lakini mwaka 2008 baba huyo na binti yake waliuamsha tena moto wa mapenzi na kuanza kuishi pamoja.
Nicola alijaribu kufanya uhusiano huu uwe wa siri akijaribu kufanya kila awezalo ili familia yake isijue kinachoendelea.
Lakini dada yake siku moja aligundua picha za ngono alizopiga Nicola na baba yake zilizokuwa kwenye simu na ndipo alipomuonyesha mama yao ambaye alihamaki kwa kusema "Huyu alikuwa mume wangu wa zamani".
Akitoa hukumu, jaji wa kesi hiyo alisema "Najua kuwa mko kwenye uhusiano uliojaa mapenzi ya kweli, lakini uhusiano huu ni kinyume na maadili ya jamii".
"Ni uhusiano usiokubalika mbele ya jamii kwa sababu ambazo zinaeleweka", aliongeza jaji huyo.
Wakati Andrew akihukumiwa kwenda jela miezi 10, Nicola alihukumiwa kwenda jela wiki 26 lakini kifungo hicho kilibadilishwa na kuwa kifungo cha nje cha miaka miwili
0 Comments