Tawi la vijana la Afrika Kusini la chama tawala cha ANC, limeomba msamaha kwa chama, kwa kuingilia kati ya maswala ya mashauri ya nchi za nje, lilipotoa wito kuwa serikali ya nchi jirani ya Botswana, iliyochaguliwa kwa njia za demokrasi, inafaa kupinduliwa.
Mapema mwezi huu, ANC ilililaumu vikali tawi lake la vijana, na kiongozi wake mkakamavu Julius Malema kwa matamshi hayo.
Ombi la msamaha la Bwana Malema lilitangazwa na redio ya taifa:

"Tuliona lazima tuombe msamaha na kufuta taarifa hiyo iliyotolewa na kamati kuu ya tawi la vijana.
Sababu ni kuwa tumeona taarifa hiyo imechafua maingiliano baina ya tawi la vijana na chama.
Kuwa na mvutano hadharani baina ya yetu na ANC ni jambo lisilokubalika; na ingefaa kujua hayo."