Watu kama 20 wamekufa katika shambulio lilofanywa na wapiganaji dhidi ya jengo la serikali, kati ya Afghanistan.
Watu waliokuwa na silaha, pamoja na washambuliaji wa kujitolea mhanga, walivamia ofisi za gavana wa jimbo la Parwan, Abdul Basir Salangi.

Mapigano yaliendelea kwa saa kadha.
Polisi, maafisa wa usalama, na washauri wa kigeni wakihudhuria mkutano hapo wakati shambulio lilipoanza.

Wadadisi wanasema michafuko imezidi hivi karibuni katika eneo hilo.