Zaidi ya miili ya watu 200 imepatikana katika hospitali iliyotelekezwa katika mji mkuu wa Libya Tripoli .

Mwandishi wa BBC ambaye alikwennda katika hospitali ya Abu Salim aliikuta miili ya wanaume ,wanawake na watoto kwenye vitanda na veranda na pia damu nyingi iliyotapakaa kwenye sakafu .

Madaktari na wauguzi walikuwa wameitoroka hospitali hiyo kufuatia mapigano.

Walionusurika wanasema wengi waliokuwa na majeraha waliachwa bila matibabu hadi kufa , huku wengine ikioza kando yao.

Katika mji mkuu wa Tripoli kuna taarifa kuhusu kupatikana kwa mamia ya miili ya watu waliouawa baadhi yao wakiwa wamekatwa mikono.

Pande mbili zinazohusika na mzozo nchini Libya zimekuwa zikilaumiwa kwa mauji hayo.