Mpango huo umetangazwa na Afisa Uhusiano wa CRDB, Medard Kayombo katika kikao cha madiwani wa halmashauri hiyo.
Kayombo alisema benki hiyo imeamua kutoa mkopo huo kwa vyama hivyo kati ya 84 vilivyopo katika halmashauri hiyo baada ya kubaini kuwa wakulima hao hawawezi kufanikiwa katika kilimo kama wanajitegemea kwa fedha zao binafsi.Alisema wakulima wamekuwa wakipata shida na hasa katika suala la malipo kutokana na kutegemea benki moja na hilo limekuwa likimsababishia madeni ambayo sasa yatapungua baada ya CRDB kuwakopesha.
Alisema CRDB itawakopesha matrekta makubwa aina ya fagurson 20 yenye thamani ya Sh.milioni 900, malori tisa aina ya Mitsubish Fuso yenye ya Sh.milioni 450 na kujenga maghala 32 yenye thamani ya Sh. bilioni 1.5.
0 Comments