Mtoto wa kiume wa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ni miongoni mwa watu 12 waliofunguliwa mashtaka ya kuhusika kwenye ghasia za baada ya uchaguzi na kusababisha vifo vya watu 3,000.
Michel Gbagbo, aliye na uraia pacha wa Kifaransa na Ivory Coast, alishtakiwa na washirika wengine wa karibu wa baba yake. Miongoni mwao ni pamoja na waziri mkuu Pascal Affi N'Guessan, mkuu wa chama cha Bw Gbagbo.
Watu hao ni miongoni mwa wengi waliopewa kifungo cha ndani na Bw Gbagbo mwezi Aprili.
Mwandishi wa BBC John James wa Abidjan alisema viongozi wote waliokamatwa na Bw Gbagbo wameshtakiwa, isipokuwa yeye Bw Gbagbo na mkewe Simone.
Watu hao 12 wanashtakiwa kwa kushiriki kwenye uasi.
Bw Gbagbo alikataa kukubali kushindwa katika uchaguzi wa Rais mwezi Novemba.
Aliondolewa madarakani baada ya majeshi yanayomtii Rais Alassane Ouattara- mshindi anayetambulika kimataifa- kuingia Abidjan na kumkamata huku akiungwa mkono na umoja wa mataifa na majeshi ya Ufaransa.
0 Comments