Baadhi ya wakaazi wa manispaa wakiwa wamepiga foleni kwa kununua sukari kwa bei nafuu ya shilingi 1,700 inayouzwa na wakala wa kiwanda cha sukari cha Kagera Bw. Amir Hamza. Bei ya sukari mkoani Kagera imekuwa ikipandishwa kiholela na wafanyabiashara wa sukari kwenye maduka kwa bei ya kilo moja kati ya shilingi 2,100 hadi 2,500.
Mmoja wawakazi wa mannispaa akiwa amebeba mfuko wa sukari baada ya kuununua toka wakala wa kiwanda cha sukari cha Kagera. Kwa sasa mkoani Kagera kuna uhaba mkubwa wa sukari unaosababishwa na baadhi ya wafanyabiashara wanaosafirisha sukari inayozalishwa na kiwanda cha sukari hicho kwenda nchini Uganda kwa njia ya magendo. Inadaiwa bei ya sukari nchini Uganda ni shilingi za kiganda 7,000. Picha na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii
0 Comments