AY.

Nyota wa muziki wa bongofleva, Ambwene Yesaya ‘AY’ na C- pwaa wanakabana vikali katika kuwania tuzo ya video bora ya Afrika Mashariki ambayo pia inapiganiwa na Mganda Keko na Wakenya Jaguar na kundi la P-Unit.
Fainali za tuzo hizo ambazo huandaliwa kila mwaka nchini Afrika Kusini na kujulikana kama ‘Channel O Music Video Award’, zinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa Oktoba. 
C-PWAA.

Video za nyimbo zitakazochuana katika tuzo hizo za wasanii wa bongofleva ni pamoja na video ya AY aliyomshirikisha Ms Trinity ‘Good Look’ na ‘Action’ aliyoimba C-pwaa, akiwshirikisha Ms. Triniti, Dully Sykes na Albert Mangwea.
Pia mashindano hayo yamemleta tena msanii wa bongofleva, ‘Shaa’ ambaye atakuwa akiwania tuzo iitwayo ‘Most gifted Afro Pop’ kupitia wimbo wake wa ‘Crazy’.