Wazee wa Pamba.

UONGOZI wa bendi ya FM Academia maarufu kama ‘Wazee wa Ngwasuma’, umesema kwamba maonesho yake ya Sikukuu ya Idd el Fitri, yatakuwa ya aina yake kutokana na mikakati yao ya kutikisa katika muziki wa dansi nchini.

Sikukuu hiyo inatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa wiki ijayo, ikiwa ni baada ya kumalizika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa Waislamu wote duniani ambao kwa kawaida huwa katika ibada hiyo kwa siku 29 au 30. 

Wacheza show wa band ya Fm Academia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha ambaye pia ni Ofisa Habari wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kwamba wanamuziki wao wanajiandaa vizuri kwa ajili ya onesho la Idd.

Alisema maandalizi hayo yanatokana na kiu yao ya kutikisa katika tasnia ya muziki huo, wakiwa na malengo ya kuwapatia burudani kubwa mashabiki wao waliozagaa sehemu mbalimbali za nchi yao.