Baadhi ya kazi FAKE zilizocopiwa tayari kwa kwenda kuuzwa kwa bei ya hasara kabisa.Yani hawa watu wamekuwa wakirudisha maendeleo ya maisha ya wasanii kila kukicha kwa kucopy kazi za wasanii kwa ubora usiohitajika na kuuza kwa bei ndogo sana.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari leo mchana,kwenye kituo cha Polisi Urafiki,mara baada ya kuwanasa watuhumiwa wa Kucopy kazi za wasanii mbalimbali,aidha aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Bashir Abdul pamoja na Jofrey Anatori (Wakazi wa Mabibo jijini Dar) .Msama alisema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo ya Mabibo Mpakani,jijini Dar,wakiwa na mitambao yao pamoja na kazi mbalimbali walizozicopy zenye thamani ya sh milioni 25.Aidha Msama amefafanua kuwa mpaka sasa wamekwisha wakamata watuhumiwa wapatao 10,wakiwa na mitambo yao,ambapo mpaka sasa wawili wamepata dhamana na wengine bado wako rumande.
Mmoja wa Watuhumiwa akiwa na vifaa vyake vya kucopy pamoja na kazi feki ambazo alikiwisha zicopy tayari kwa kuzipeleka sokoni.Baadhi ya kazi feki zilizokamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Mabibo Mpakani,jijini Dar na kampuni ya Msama Auction Mart. (source Michuzi)
0 Comments