Wakazi wa Igunga wakiwa wameizunguka helikopta ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambayo inasaidia kampeni za chama hicho katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo. Helikopta hiyo ilitua karibu na ofisi za chama hicho ikiwa njiani kuelekea kwenye mkutano wa kampeni jana.