Nyumbani watu wanatangaziwa kilimo kwanza wanazembea,hawajui kilimo ni uti wa mgongo?Hiki ni kijishamba kilichopo pembeni mwa nyumbani ninapoishi.
Kimfaacho mtu chake,naingia katika kijishamba cha mahindi kuangalia mahindi ya kuchemsha na familia yangu nyumbani.
Nachagua wajameni,maana ukichuma mateke sana unakuwa unaharibu mambo lazima uchume yaliyokomaa kidogo.
Nachuma kulingana na idadi ya watu nyunbani,maana nikichuma mengi sana yatabaki kisha nitakuwa nimeharibu chakula.kwahiyo hapo nahesabu kila mmoja atakula mangapi...
La mwisho hiloooo,naenda zangu nyumbani kuchemsha sasa.Unabisha Mnyamwezi hawezi kuacha asili yake? kama unabisha subiri hiyo siku ya kuona Asali,viazi vitamu na karanga kwa pembeni hapo ndipo utajua kuwa wanyamwezi hawana kuacha asili hata wawe Majuu.
0 Comments