Bwana Onyango Obama alikamatwa wiki iliyopita kwenye mji wa Framingham karibu na Boston baada ya kusimamishwa na polisi kutokana na kuvunja sheria za usalama barabarani.

Onyango alipelekwa kituo cha polisi baada ya kugundlika kuwa alikuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa.

Alipopewa ruhusa ya kupiga simu kuwaatarifu ndugu zake, Onyango mwenye umri wa miaka 67 aliwaambia polisi "Nafikiri itanibidi nipige simu White House (ikulu ya Marekani)".

Onyango aliendelea kushikiliwa na polisi bila ya kupewa dhamana huku maofisa wa uhamiaji wakimchunguza uhalali wake wa kuishi Marekani kwakuwa Onyango katika miaka iliyopita aliwahi kuamriwa na mahakama aondoke nchini Marekani.

Polisi wa Marekani walithibitisha kuwa Onyango ambaye asili yake ni Kenya ni kaka wa baba yake Obama na pia ni kaka wa shangazi yake Obama, Zeituni Onyango ambaye jina lake lilitamba sana kwenye magazeti ya Marekani mwaka jana baada ya kushinda

kesi na kuruhusiwa kuishi Marekani na hivyo kuepuka amri iliyotolewa awali na mahakama kuwa arudishwe kwao Kenya.
chanzo cha habari toka http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=5916070&&Cat=2