Rais Obama na mawazo Lukuki.
Idadi ya raia wa Marekani wanaoishi katika umaskini imeongezeka hadi watu milioni 46.2 mwaka uliopita,kwa mujibu wa idara ya kuhesabu watu Marekani,karibu mtu mmoja kati ya raia sita,wanaishi katika hali hiyo.
Huyu mtu hana pakulala.
Takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa umaskini umeongezeka hadi asilimia 15.1%,kutoka 14.3% mwaka 2009.Idadi ya raia wa Marekani wasio na bima ya afya pia imepanda hadi milioni 49.9.
Raia wa Marekani wakiwa wamepanga foleni kusubiri kupata msaada wa chakula.
Kiwango cha umaskini kimeongezeka kwa mfululizo
Kiwango hiki cha umaskini ndicho cha juu zaidi tangu mwaka 1983,na ni sawa ya mwaka 1993.
Idadi ya raia wa Marekani wanaoishi katika hali ya umaskini sasa imeongezeka kwa miaka minne mfululizo.
Wamarekani weusi na wenye asili ya uhispania waathirika zaidi
Tafsiri ya umaskini nchini Marekani ni kuwa na kipato cha dola $22,314 kila mwaka,au chini yake kwa familia ya watu wanne,na dola $11,139 kwa mtu mmoja.
Idara hiyo ya kuhesabu watu pia imeonyesha kuwa umaskini miongoni mwa raia wa Marekani weusi na wenye asili ya kihispania iko juu zaidi katika mwaka uliopita-asilimia 27.4% na 26.6% mtawalia. http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2011/09/110914_marekani_umaskini.shtml
0 Comments