Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy

Mkuu wa baraza la kitaifa la mpito nchini Libya ameomba vikosi vyake vipewe silaha ili waongeze juhudi zao za kuteka maeneoe mengine ya nchi ambayo yamedhibitiwa na wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi.

Mustafa Abdul Jalil ameambia BBC kwamba kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani yuko kusini mwa Libya na anapanga kufanya mashambulio.

Ujumbe uliondikwa na unasemekana umetoka kwa Gaddafi umeomba Umoja wa Mataifa kusitisha "uhalifu'' dhidi ya eneo alilozaliwa la Sirte.

Wakati huo huo, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anafanya ziara katika mji wa Tripoli siku ya Alhamisi.

Marekani imeridhishwa na utawala mpya wa Libya


" Tunawaambia viongozi wanaokuja kuwa watakuwa salama," Bwana Abdul Jalil alisema. Hakusema kiongozi gani mwingine wa kigeni ataongozana na Rais Sarkozy.

Hata hivyo, mwanafalsafa wa Ufaransa Bernard-Henri Levy, aliyeshinikiza jamii ya kimataifa kuvamia Libya, atakuwepo kwenye ziara ya Tripoli.

Mapema, Marekani ilisema kuwa imeridhishwa na jinsi baraza hilo la mpito linavyowea kudhibiti vikosi vya usalama nchini.


'makabiliano makali'



Vikosi vinavyomuunga mkono Gaddafi bado vinadhibiti maeneo manne, ikiwemo Sirte, na Bani Walid, kusini-mashariki mwa mji mkuu Tripoli, pamoja na Jufra na Sabha.

Bwana Abdul Jalil anasema wengi ya wale wanaomuunga mkono Gaddafi wamekimbia hadi Sabha katika jangwa lililoko upande kusini.

Gaddafi anamiliki dhahabu yote


" Kutakuwa na makabiliano makali Sabha na vifaa kwa sasa hatuna, na tunaomba vifaa zaidi ili tuweze kuchukua udhibiti tena wa haya maeneo," amesema Bwana Abdul Jalil.

Alisema Gaddafi anamiliki "dhahabu yote" na atapanga mashambulio katika miji, visima vya mafuta na mitambo ya umeme.