Kiongozi wa baraza la mpito nchini Libya ametoa wito kwa watu wa Libya kujenga jamii yenye kuvumiliana na inayoheshimu utawala wa sheria.
Akizungumza katika mkutano huo wa Paris huko ufaransa kiongozi wa baraza la mpito la Libya Abdel Jalil ameahidi kwa Libya itakuwa na katiba mpya katika kipindi cha miezi 18 ijayo.
Amesema baadae baraza lake litaandaa uchaguzi katika misingi ya kidemokrasia.
Jalil amesisitiza kuwa ujukumu la kujenga Libya ni la walibya wenyewe.
Nae mwenyeji wa mkutano huo Rais , Nicolas Sarkozy wa Ufaransa aliuambia mkutano huo kuwa kazi iliyo membe ya jamii ya kimatiafa ni ya kuijenga upya Libya.
Hata hivyo Sarkozy amesema kuwa Mashambulizi ya NATO kwa kutumia ndege bado ya taendelezwa hadi pale watakapo hakikisha kuwa Kanali Muamar Gaddaifi sio tishio tena kwa Libya.
Na Katibu mkuu wa Baraza la Umoja wa Matifa Ban Ki Moon amesema kwa wakati huu jambo linalofaa kushughulikiwa kwa dharura ni kuhakikisha kuwa Libya kuna madawa, mafuta , maji na chakula cha kutosha.
Baada ya kufanya mkutano wa faragha na kiongozi wa mpito wa Libya, Rais wa Senegal Abdoulaye Wade aliuomba Umoja wa Afrika kutambua na kulikubali bazara la mpito la Libya.
0 Comments