Mtoto mwenye malaria akiwa amelala hospitali


Watafiti wana mpango wa kuendelea kuifanyia kazi jaribio ya kinga mpya ya malaria baada ya kuibuka matokeo yenye matumaini katika utafiti wa awali nchini Burkina Faso.

Jaribio hilo lilibuniwa kupima usalama, lakini watafiti waligundua kwamba watoto waliopewa kinga walikuwa na kiwango kikubwa cha kinga.


Ikielezwa kuwa ni matokeo "yenye kutia moyo", utafiti mkubwa zaidi utakaohusisha watoto 800 unatarajiwa sasa kufanyika nchini Mali.

Wanasayansi waliohusika wanasema wana matumaini kuwa kinga hiyo itaweza kutengenezwa kwa gharama ndogo.

Takriban kinga 100 za malaria zimetengenezwa mpaka sasa lakini MSP3 iliyofanyiwa majaribio Burkiina Faso ni ya pili ambayo angalau imeonyesha kiwango cha kutoa ulinzi dhidi ya ugonjwa huo.

Utafiti huo ambao haukuwa na utaratibu maalum, uliwahusisha watoto 45.

Ilikusudia kupima usalama wa kinga hiyo lakini utafiti uliofuatia uligundua watoto waliopewa kinga hiyo waliumwa malaria mara tatu mpaka nne pungufu ya wale ambao hawakupata.