WEMA Isaac Sepetu, Jumatano iliyopita ilikuwa siku ngumu mno kwake na kama si jitihada za mzazi, leo yangekuwa yanazungumzwa mengine.
Wema ambaye hana historia ya kumlilia mwanaume, amekamatika kwenye penzi la brazameni anayedatisha ‘maduu’, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumatano iliyopita baada ya kuambiwa anaachwa, aliona bora ajisalimishe kaburini kwa kunywa sumu.
Busara za mama mzazi wa Diamond, Sanura Khassim ‘Sandra’ ziliokoa jahazi kwa kumlazimisha mwanaye arudiane na Wema ili mambo yasiharibike.
WEMA ALIVYODATA
Jumatano iliyopita mchana, Wema alipata taarifa kuwa Diamond ‘Platinumz’ alishazungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza uamuzi wake wa kumuacha jumla.
Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006-07, alipata taarifa hizo akiwa kwenye kambi ya kurekodi filamu kwenye Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam.
Mdada wa nguvu Wema Sepetu.
Tukio la kwanza, Wema alivua pete ya uchumba aliyovalishwa na Diamond kwa hasira, akaanza kulia.
Baada ya kutafakari, Wema aliona mtetezi pekee ni mama mkwe wake, Sandra, hivyo alimpigia simu na kuangusha kilio cha “mama mkwe nisaidie mwanao asiniache.”
Utu uzima dawa, Sandra alimwita mrembo huyo nyumbani kwake, Sinza, Dar ili wazungumze. Mapenzi ya Diamond ndani ya Wema, yana nguvu kuliko kazi, kwa hiyo akaondoka kambini bila kurekodi na kumuacha prodyuza wa muvi hiyo, Suleiman Barafu akiwa na mshangao.
Barafu alikasirika lakini wasanii wenzake, walimshauri amvumilie Wema kwa sababu yupo kwenye mateso makubwa ya kimapenzi.
Wema alipofika nyumbani, alimvamia mama mkwe wake, ‘mchozi’ huo, akamlamba miguu, akasema: “Mama nampenda Diamond kuliko chochote, akiniacha sina pa’ kuweka sura yangu.”
Akamchanganya mama mkwe: “Sitanii mama, endapo Diamond ataniacha, sitakuwa na uwezo wa kubeba haya mapenzi makubwa niliyonayo. Nitakunywa sumu, nitakufa. Ila sitajali kwa sababu nitakufa kwa sababu ya penzi la mwanaume ninayempenda.”
Mama Diamond ‘Sandra’ kusikia hivyo, akapagawa: “Mkamwana afe juu ya nini?” Alimwita Diamond nyumbani wazungumze lakini muafaka haukupatikana.
KIKAO USIKU MZIMA TABATA
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda linajitosheleza kwa data kwamba Sandra alimlazimisha Diamond arudiane na Wema ili kuokoa uhai wa mrembo huyo.Kwa Diamond, ilikuwa ngumu kukubali, akishusha madai kuwa Wema ni mvivu, hapiki chakula nyumbani, hafui nguo, kazi zote hizo zinafanywa na mama yake (Sandra). Ameshasikia mengi lakini siyo ishu, kubwa ni kwamba mrembo huyo anamlazimisha Platinumz amfukuze mama yake mzazi ili wawe huru.
Hata hivyo, mama mtu alipangua hoja za Diamond na kuwataka wamalize tofauti zao na kurudiana.
Kikao hakikuzaa matunda, saa sita usiku (Alhamisi), Diamond, mama yake, mjomba wake anayeitwa Saidi na kaka yake aliyefahamika kwa jina la Hamisi, walizungumza kwa muda mrefu kuhusu hatima ya mastaa hao.
BUSARA ZA KIUTU UZIMA
Habari zinasema kuwa baada ya mvutano wa muda mrefu, Saidi na Hamisi walisimama upande wa Sandra, hivyo kushinikiza Diamond kurudiana na Wema.
Kutokana na shinikizo hilo, Diamond alinywea, akasalimu amri mbele ya wakubwa.
WEMA KAFICHWA
Kumpata Wema kwa sasa ni kazi ngumu kuliko kumtafuta Mullah Omar, kwani simu yake imezimwa na vyanzo vyetu vimetutonya kuwa mrembo huyo amekatazwa na Diamond asizungumze chochote kwa rafiki zake wala kwa chombo chochote cha habari.
NENO LA DIAMOND
Gazeti hili lilizungumza na staa huyo Ijumaa akiwa Dodoma, alikokwenda kufanya shoo, hili ni jibu lake: “Ni kweli, mimi na Wema tumerudiana. Mama alishinikiza, kwa hiyo nikasalimu amri.”
KAULI YA FAMILIA
Mama wa Diamond hakupatikana lakini kaka yake, Hamisi alisema: “Dogo alikosea kumuacha mwenzake bila kumshirikisha mzazi wake.”
KWELI WEMA KANASA
Wema alishaachana na wanaume kadhaa ambao walibaki na sononeko, yeye hakujuta na alisonga mbele lakini kwa Diamond imekuwa tofauti.
Baadhi ya wanaume hao ni wasanii, Steven Charles Kanumba, Charles Gabriel Mbwana, Hartmann Osmund Mbilinyi na Jumbe Yusuf Jumbe.
3 Comments
Bro Maganga hukumbania anonymous wa 30october na mi usinibanie
Bro Maganga hukumbania anonymous wa 30october na mi usinibanie. Farida Kombo