Serikali ya Bahrain imekiri kua vikosi vyake vilikiuka haki za binadamu, ingawa imeongezea kua visa hivyo havikufanywa kwa kubagua na kwamba waandamanaji nao watalaumiwa kwa kuchangia katika uhalifu.

Kamati iliyoidhinishwa na Mfalme Hamad bin Al Khalifa(pichani kushoto) kuchunguza visa vya ukiUkwaji wa haki za binadamu kufuatia malalamiko 8000, ni pamoja na visa vya ubakaji na kuwanyanyasa waandamanaji inatazamiwa kutangaza ichunguzi wake mwishoni mwa mwezi huu.Waziri wa Afya na haki za binadamu, Bi.Fatma Al-Baluchi, ameiambia BBC kua serikali yake inakubali kuwa haki za binadamu zilivunjwa katika harakati za serikali za kukabiliana na waandamanaji mwaka huu lakini akaongezea kuwa hali hiyo haikupangwa.
Taifa linalopitia kipindi kigumu la Bahrain linakabiliwa na wakati wa kufikia uwamuzi. Baada ya kipindi cha miezi minane ambapo ghasia kali zimejitokeza, tume huru ya Bahrain inatazamiwa kutangaza uchunguzi wake ifikapo tareh 30 oktoba.


Kamati iliyoidhinishwa na Mfalme lakini inaongozwa na wanasheria wenye sifa na wa Kimataifa, wachunguzi wake wametizama zaidi ya malalamiko 8800 na kuwahoji wahusika wasiopungua 5000.

Wamesema kua walipewa uhuru na serikali na kwamba hawajakabiliwa na uingiliaji kati wa serikali wala kikwazo cha aina yoyote.

Lakini katika jamii hii yenye chuki ambapo wafuasi wa madhehebu ya Washia wenye idadi kubwa kuliko wengine, na ambao wanadai mgao sawa wa mapato ya dola, ardhi na madaraka, wanadai kuwa huenda Kamati ikapendelea serikali na kuiondolea lawama na kwa hiyo ubaguzi dhidi ya Washia utaendelea.