Waziri wa ulinzi wa Uingereza Liam Fox(pichani kushoto) amejiuzulu baada ya chagizo za wiki nzima kuhusu uhusiano wake na rafiki yake na mtu aliyejiita kua ni mshauri wake Adam Werritty.
Bwana Fox alikua anapelelezwa kuhusu madai kwamba alivunja itifaki za kiwaziri.
Katika barua kwa David Cameron, Bw Fox alisema "nilikosea kuruhusu majukumu yangu ya kibinafsi kuingiliana na majukumu ya kikazi ".
Katika jawabu yake , Waziri Mkuu alisema amesikitishwa kuona Bw.Fox akiondoka lakini anaelewa sababu zake.
Chama cha upinzani cha Labour kimesema Bw Fox hakutekeleza hadhi inayotarajiwa kutoka kwa mawaziri na kuondoka kwake kulikua lazima.
Waziri huyo wa ulinzi amekua akikabiliwa na shinikizo ajiuzulu tangu ilipobainika kuwa rafiki yake Bw.Werritty, amekutana nae mara 18 katika safri za ngambo licha ya kutokua na jukumu rasmi na amekua akitawanya kadi za kujitambulisha kama ni mshauri wa Bw Fox.
Maswala kadhaa yamekua yakiuzuliwa kuhusu nani aliyelipia shughuli za kibiashara za Bwana Werritty na kama alifaidika moja kwa moja kutokana na mikutano yake ya mara kwa mara na waziri wa ulinzi.
0 Comments