Watoto wa jinsia zote wa familia ya kifalme nchini Uingereza sasa watakuwa na haki sawa kutawala.
Viongozi wa Jumuiya ya madola wamefanya mabadiliko ya sheria za kurithishana utawala wa kifalme.
Viongozi hao kutoka nchi 16 za Jumuiya hiyo ambako Malkia ni mkuu wa nchi kwa pamoja wamepitisha mabadiliko hayo katika mkutano wao huko Perth, Australia.
Ina maana kuwa mtoto wa kwanza wa kike wa mwana wa mfalme na mkewe (Duke and Duchess of Cambridge) atachukua nafasi ya ndugu zake wa kiume watakaozaliwa.
Amri ya kuizuia familia ya Kifalme kuoa au kuolewa na Mkatoliki imeondolewa.