Habari zenu wapenzi na wasomaji wetu.
Wiki iliyopita tualianza kwa kuzungumzia sifa na vigezo vya wanawake vinavyoleta mvuto kwa wanaume
Kuna sifa nyingi sana ambazo mwanaume uvutiwa na mwanamke pindi amuonapo.Moja ya sifa kuu kabisa ni
MVUTO WA SURA
wanawake wote duniani hakuna hata mmoja utakayesema ni mwanamke mbaya wote ni wazuri,ila wamezidiana uzuri wao kimuonekano machoni mwa wanaume.



Mwanamke yoyote mwenye sura nzuri huwa ni kivutio cha kwanza kwa mwanaume kabla hajaanza kushughulikia masuala mengine ya kuuchambua uzuri na sifa za mwanamke huyo.Uzuri za sura ya mwanamke inategemea na jinsi alivyo,kwanza kabisa kuna wale wenye sura nzuri asilia na kuna wale wenye uzuri wa sura kwa kujitengeneza.
Uzuri wa sura asilia,kuna wanawake wengi sana ambao sura zao ni nzuri sana na pindi akitokeza machoni mwa wanaume kila mmoja uacha anachokifanya na kupoteza japo dakika kadhaa ili kuangalia uzuri wa msichana au mwanamke huyo.kuna uzuri mwingine wa kujiremba,kadhalika nao pia uchengua akili za wanaume inategemea tu ni jinsi gani mwanamke huyo amejiremba.Hivyo basi wanawake lazima mjue jinsi ya kujiremba kwani kujiremba kwenu ni moja ya vivutio kwa wanaume.
MVUTO WA UMBILE
Kama ilivyo ada duniani,kuna wanaume wachache sana duniani ambao hawaangalii maumbile ya wanawake ila wengi wao hupendelea kuchagua wanawake wenye maumbile mazuri pindi watembeapo wafurahie mvuto wa mwanamke.Umbile la mwanamke ni kigezo kiukubwa sana kwa mwanaume,kuna wanawake waliozaliwa na maumbile mazuri na yenye mvuto na kuna wanawake wengine ambao wanatengeneza maumbili yao na kuonekana mazuri kutokana na mazoezi au mambo mengineyo yatakayowaletea mvuto fulani.hivyo ni vyema wanawake mkae mkijua kuwa mnapokuwa mnakula vyakula vyenu ni lazima mzingatie mambo ya diet ili kuweka sawa maumbile yenu.umbile la mwanamke ni sumaku kwa mwanaume.
MAZUNGUMZO
Wanawake wengi siku hizi wamekuwa na tabia za kutokuona haya pindi wakutanapo na wanaume,dunia ya sasa imewageuza wasichana wengi kutokuwa na haya na matokeo yake wanakosa zilie percent ambazo mwanamke anastahili kuwa nazo.kwa kawaida msichana ambaye hana haya mwanaume huwa hapendelei kuwa nae hata kama ni mzuri vipi.msichana anayepaza sauti wakati wa maongezi,msichana ambaye ana matusi mbele za watu,msichana mwenye kupenda kubishana mbele za watu.na msichana ambaye anataka kuonekana yupo juu zaidi mbele ya wanaume,kiufupi wasichana wengi wanajikosesha bahati kwa tabia mbaya mbele za wanaume.
UCHESHI
Kuna baadhi ya wasichana ni wacheshi na ucheshi wao unategemea ni mahala gani pa kufanya ucheshi wao.ni sifa nzuri msichana kuwa na ucheshi ila ucheshi wake inategemea aufanye mahala gani.kwa kawaida hakuna binaadamu hasiyependa furaha,ila kuna baadhi ya wasicha ucheshi wao unapi.........tukutane tena wiki ijayo. Nakaribisha maoni kupitia magangaone@gmail.com au gonga hapa chini kwenye sehemu iliyoandikwa neno maoni.