Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa (kushoto) akimsaidia Kada wa CCM, Mustafa Sabodo kunyanyuka kwenye kiti nyumbani kwa kada huyo Upanga, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Jamson

-AMWAGA MABILIONI KUCHIMBA VISIMA, ASIFU MSIMAMO WA DK SLAA
KADA wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi kuchimba visima 200 katika majimbo yote ya wabunge wa Chadema nchini, huku akieleza kuwa angependa kuona upinzani unachukua nchi mwaka 2015.Sabodo ambaye ni kada wa CCM tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyarere, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akipokea mpango wa uchimbaji visima hivyo kutoka kwa Katibu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.Kauli hiyo ya Sabodo ambaye tayari katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana aliisaidia Chadema Sh100 milioni za kampeni.