Maiti ya Wangari Maathai imechomwa moto mjini Nairobi, kama alivyousia.

Kabla ya hapo Bibi Maathai, aliyefarika mwezi uliopita kutokana na saratani, aliagwa kwa maziko ya kitaifa.

Bibi Maathai aliwahi kupata tuzo ya amani ya Nobel, na alikuwa maarufu kwa kazi yake ya kutetea wanawake na mazingira.

Kabla ya hapo Bibi Maathai, aliyefarika mwezi uliopita kutokana na saratani, aliagwa kwa maziko ya kitaifa.

Bibi Maathai aliwahi kupata tuzo ya amani ya Nobel, na alikuwa maarufu kwa kazi yake ya kutetea wanawake na mazingira.

Wanaharakati wa mazingira na wanawake ambao walishirikiana na Bibi Maathai tangu alipoanza kampeni zake miaka ya 1970 piya walihudhuria, pamoja na wawakilishi kutoka nchi za nje.

Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Makaazi, Bibi Anna Tibaijuka, ambaye piya alikuwa rafiki wa Bibi Maathai; Sudan ilituma mwakilishi, na wanabalozi wa nchi kadha walihudhuria.

Baadhi ya waombolezi walibeba miche ya miti ili kuipandisha hapo bustanini; na familia yake iliotesha mti wa kiasili ili kubakisha kumbu-kumbu ya marehemu.


Kukumbuka msimamo wake wa kutotaka miti kukatwa, jeneza lake limetengenezwa kwa magugu ya majini, kili, na mwanzi

Katika miaka ya 1970 Bibi Wangari Maathai alianzisha shirika la Greenbelt Movement, ambalo lengo lake lilikuwa kuwapunguzia shida akina mama, ili waweze kupata kuni na maji safi kwa urahisi.

Tangu wakati huo karibu miti milioni 50 imepandishwa Kenya.

Maelfu itapandishwa siku zijazo kama kumbukumbu kwa mawanamke aliyegusa nyoyo za watu wa Kenya na dunia nzima.

Bibi Maathai piya alipigania wafungwa wa kisiasa waachiliwe.