Mwanaharakati wetu mzalendo Jessica Mushala ambae alikuwa Mc kwa siku ya jana katika kongamano zima la kumbu kumbu la kumkumbuka Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika Georgia Avenue, Washington DC nchini Marekani.
Baadhi ya wanachama wa Julius K. Nyerere Commemoration waliohudhuria katika kumbu kumbu ya kumkumbuka Baba wa Taifa.
Washiriki wa Julius K. Nyerere Commemoration, Inc. wakimsikiliza kwa makini baadhi ya mambo muhimu yaliyokuwa yakielezewa ukumbini hapo.
Mjukuu wa Baba wa Taifa, Hellena (kushoto) akiwa na Mama yake Leticia M. Nyerere (katikati) na Mariam wa Bahari Deco Crafts,(kulia) kwenye kumbu kumbu za kumkumbuka Mwalimu Julius K Nyerere zilizofanyika jana jijini Washington nchini Marekani.
Wanafunzi waliotumbuiza kwa kuimba kiswahili pamoja na kizulu walipendezesha kumbukumbu za kumuenzi baba wa taifa ukumbini hapo.kila mmoja alifurahia uimbaji wao.
Pichani kushoto ni swahiba wangu na mmiliki wa swahili villa blog ambaye alipata bahati ya kupiga picha ya pamoja na Leticia M. Nyerere katika shughuli nzima ya kongamano la kumuenzi baba wa taifa jana jijini Washington nchini Marekani.Katika maongezi yao mmiliki huyo wa Swahili Villa bwana Abou Shatry alimtambulisha bidada Leticia shughuli zinazofanyika katika blog yake ya Swahili Villa.kwa mapicha kedekede ya shughuli nzima ya jana tembelea http://swahilivilla.blogspot.com
0 Comments