Katika hali isiyo ya kawaida, mwanamke mmoja mkoani Rukwa amejifungua mtoto anayefanana na samaki aina ya nguva katika hospital ya Dokta Atimani, Manispaa ya Sumbawanga Mjini.
Mtoto huyo alizaliwa akiwa hai na kufariki muda mchache baada ya kapewa huduma za awali anazopewa mtoto anapozaliwa.
Akitoa maelezo yake mkunga aliyemzalisha mama huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwanzunga, alisema kuwa ni tukio la aina yake kwake kuliona na kwamba hii ni mara ya pili kutokea katika hospitali hiyo kwa kuzaliwa watoto wanaokua na maumbile tofauti na binadamu.
Alisema kuwa mtoto huyo alikuwa na sura ya binadamu mikono miwili na alikuwa ameungana kutoka kiunoni hadi miguuni hali iliyosababisha kutengeneza umbo la samaki mtu.
Alisema kuwa kiumbe hicho kilikuwa na jinsia iliyoshindwa kutambulika kama ni mwanamke au mwanaume na njia ya haja kubwa ilikua imekaa juu ya kiuno katika mgongo wake.
Pia alisema kuwa mtoto huyo alikuwa na uwezo wa kuuinua mkia wake na kuukunja hadi kichwani ambapo alikuwa akificha uso wake usionekane na kisha kuugeuza hadi kisogoni.
Pia alikuwa na nywele za kawaida ndefu na nyeusi hali iliyowafanya watu kushangaa, na alifanya hivyo mfululizo kujigeuza na kujificha hadi alipofariki dunia.
Mganga Mkuu wa hospitali alithibitisha kutokea tukio hilo.