Wakizungumza jana, mbunge huyo Moses Machali na wananchi mbali mbali kutoka mkoani Kigoma wamekiri kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na Precision Air karibu miezi miwili iliyopita sasa imefanya usafiri wa abiria kuingia na kutoka mkoani humo kuaminika na wakutegemewa zaidi.
Akihojiwa kwa njia ya simu Mbunge wa Kasulu Mjini Moses Machali alisema, “Kwanza nichukue fursa hii kuwapongeza Precision Air kwa uamuzi wao wa kurejesha safari hizi, maana tangu ATCL wajitoe safari za kuja na kutoka huku usafiri ulikuwa wa shida sana.”
Aliendelea, “Hivi sasa usafiri wa shirika hili inatusaidia sisi wabunge, maafisa wa serikali, wafanyabiashara na hata wananchi wa kawaida kutekeleza majukumu yetu kwa uhakika na kwa ufanisi zaidi.”
“Muda ni mali,” alisisitiza.
Akizungumzia upande wa bei Mbunge huyo wa Kasulu Mjini alisema kwamba kabla ya Precision Air kuingia katika soko la Kigoma gharama za usafiri zilikuwa za juu mno, tofauti na sasa ambapo gharama zimepungua na kwa kiasi kikubwa imepunguza kero kwa mwananchi.
Akizungumzia faida za kupitia Mwanza kutokea Kigoma Meneja Mauzo huyo alisema kwamba inatoa fursa kwa abiria kutokea Kigoma kuwa na uwezo wa kuunganisha safari zingine za shirika hilo zinazoelekea sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi kama Arusha, Musoma, Entebbe, Nairobi na kadhalika.
Kwa upande mwingine Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali ametoa wito kwa shirika hilo kufikiria safari za kwenda Dodoma ili kuiunganisha makao makuu hayo na sehemu zingine za nchi.
0 Comments