Pichani kati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Links Ltd,Mohamed Bawazir ambaye ndiye muandaaji wa pambano la ubingwa wa UBO INTER-CONTINENTAL BANTAM WEIGHT,akizungumza mapema leo asubuhi kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya JB BELMONTE HOTEL,jijini Dar kuhusiana na pambano hilo litakalokuwa la aina yake. Bawazir amesema kuwa pambano hilo litawahusisha mabondia Mbwana Matumla pichani kulia na Francis Miyayusho pichani shoto,ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 30 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar,aidha katika mpambano huo wa kukata na shoka kiingilio kimepangwa kuwa kati ya 10,000 na 5000 kwa kila kichwa. Bawazir amesema kuwa katika pambano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Kamishna wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam,Kamanda Suleiman Kova.Mbali ya mpambano huo,Bawazir alitanabaisha kuwa pia kutakuwepo na mapambano mengine ya utangulizi likiwemo pambano la akina Dada Asha Ngedere na Salma Kiombwa.
0 Comments