NA MUSA MATEJA(Global Publishers)

 IMEFAHAMIKA kuwa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ amemtundika mimba Wema Isaac Sepetu, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza kukuhabarisha.

Kipo chanzo makini cha kuaminika kilicho karibu na wawili hao ambacho kilidai kuwa kwa sasa Wema hachezi mbali na maembe mabichi, ubuyu na ndimu vinavyomsaidia kuondoa kichefuchefu.

Chanzo hicho kilidai kuwa ujauzito huo ndio uliosaidia kumaliza ugomvi wao kwa sababu pande zote mbili zilizingatia malezi ya mtoto mtarajiwa.

Ilidaiwa kuwa taarifa hizo zilipotua nyumbani kwa mama Wema, Miriam Sepetu aligeuka mbogo akidai kuwa hataki mtoto wa nje ya ndoa.

Hata hivyo, mmoja wa mapaparazi wa Risasi Mchanganyiko alitinga nyumbani kwa mama Wema maeneo ya Sinza-Mori, Dar es Salaam juzi Jumatatu na kutaka kuhojiana naye zaidi, lakini mzazi huyo akasema angefanya hivyo pindi Wema atakapofika nyumbani hapo.

Alisema Wema aliahidi kurejea nyumbani kwao siku hiyo kabla ya alasiri na kwamba angempigia simu atakapofika, lakini hadi siku inakatika hakufanya hivyo.

MAZUNGUMZO YA CHANZO CHA HABARI NA RISASI MCHANGANYIKO
Chanzo: Haloo, hapo ni Risasi?
Risasi Mchanganyiko: Naam, hujakosea.

Chanzo: Nina habari yangu lakini naomba msinitaje jina.
Risasi Mchanganyiko: Sasa tutaiandikaje bila kukutaja jina?

Chanzo: Simaanishi inanihusu mimi. Habari yenyewe ni ya staa mkubwa Bongo, nilikuwa namaanisha msiseme kama mimi ndiye nimewapa.
Risasi Mchanganyiko: Ooh! Staa gani huyo?

Chanzo: Lakini si mna habari?



Risasi Mchanganyiko: Habari zipo kibao, soma magazeti ya Global Publishers, lakini hata hiyo ya kwako ni ya muhimu kwetu.

Chanzo: Kwa taarifa yenu Diamond kampa Wema mimba na sasa ina takribani mwezi mmoja na nusu, sema tu haionekani kwa sababu kitumbo hakijaanza kutoka.
Risasi Mchanganyiko: Una uhakika?

Chanzo: Nasema kweli, sijawahi kusema uongo hata siku moja.
Risasi Mchanganyiko: Wewe umepata wapi hizo habari?

Chanzo: Mbona mimi na Wema sana tu! Hata siku alipokwenda kupima aliniambia kwa kinywa chake kuwa amenasa na mhusika ni Diamond.
Risasi Mchanganyiko: Tunashukuru kwa taarifa yako, ngoja tuifanyie kazi.

WEMA ATAKA DIAMOND ATHIBITISHE
Baada ya kukusanya data kutoka kwa vyanzo vingine tofauti, gazeti hili lilimtafuta Wema ili kupata mzani wa habari hiyo ambapo mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;

Risasi Mchanganyiko: Haloo Wema, kwanza hongera sana.
Wema: Hongera ya nini tena?

Risasi Mchanyiko: Taarifa zilizojaa tele kwenye meza ya gazeti hili zinasema umepachikwa kibendi na Diamond, je, ni kweli?
Wema: Duh! Ama kweli mnanusa mambo ya watu, siwezi kulizungumzia hilo hadi nijadiliane na baby wangu (Diamond).

Risasi Mchanganyiko: Upo naye hapo?
Wema: Huyu hapa, zungumza naye.

Risasi Mchanganyiko: Mambo vipi Diamond, je, ni kweli Wema mjamzito?
Diamond: Teh… teh… teh…! Hebu zungumza naye mwenyewe, huyu hapa.

Risasi Mchanganyiko: Wema hebu funguka.

WEMA WERAWERA
Wema: Wera…weraaaa… Ni kweli, lakini ni mapema sana kuongelea suala hili, mimi sikupanga kuliweka wazi na ningependa hasa aongee Diamond maana yeye ndiye mmiliki halali wa mimba hii, lakini kwa kuwa amenipa nafasi, nathibitisha kuwa nina ujauzito wa mwezi mmoja na nusu.

Hivi karibuni, Diamond alitangaza kummwaga Wema hivyo mrembo huyo aliingia kwenye stress ya ajabu hadi akahofiwa kujiua lakini baadaye waliweka mambo sawa wakarejesha uhusiano wao kama kawa.

Maganga One Blog inawapongeza wote kwa kurudisha uhusiano wao na inawaombea dua wapate mtoto wa baraka.