Rais wa Sudan Omar al-Bashir anasema nchi yake ilitoa msaada wa kijeshi kwa wapinzani wa Libya waliomuondoa madarakani Kanali Muammar Gaddafi.

Katika hotuba kupitia televisheni, Bwana Bashir amesema hatua hiyo ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa Gaddafi kutokana na yeye kuwaunga mkono waasi wa Sudan miaka mitatu iliopita.
Sudan na Libya hawajakuwa na uhusiano mzuri kwa miaka mingi.

Libya ilitangazwa kuwa huru siku ya Jumapili, siku mbili baada ya kifo cha Kanali Gaddafi.

'wakati wa kulipiza'

Rais Bashir anasema kundi la Justice and Equality Movement (JEM), ambalo ni la waasi kutoka eneo la Darfur, lilivamia Khartoum miaka mitatu iliopita wakitumia magari ya jeshi la Libya, vifaa, silaha, na pesa.


Anasema kuwa Mungu amewapa Sudan fursa ya kulipiza mashambulio, kwa kutuma silaha, na msaada kwa raia kwa utawala uliofanya mapinduzi.