(kama picha inavyooneka hapo juu).
Bwana Mussa ni mlinzi katika nyumba ya Joseph Mwakyusa huko Tabata. Majambazi yalipofika nyumbani kwa bawana
Mwakyusa yalimjeruhi
kwa shoka bwana mussa na, wakati majambazi yaliyovamia nyumba ya Mwakyusa yakiendelea kufungua spea za gari aina ya Toyota verosa. kwa bahati nzuri bwana Mwakyusa alishtuka
na ndipo
majambazi hayo yalipokimbia na kutoweka yakimuacha mussa katika hali mbaya na shoka ikiwa imenasa kichwani.
Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa
mahututi. bwana.
Jumaa Almasi afisa uhusiano mkuu wa MOI amethibitisha tukio hilo na kusema ''Ni kweli bwana Mussa amepokelewa hapa MOI akiwa na shoka iliyonasia
kichwani mwake lakini madaktari wamemfanyia upasuaji na kuitoa na sasa hivi yupo chumba cha wagonjwa mahututi''
0 Comments