Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotangazwa nchini Afghanistan inasema kua wafungwa katika baadhi ya jela zinazoendeshwa na nchi hio wamekua wakinyanyaswa. Madai haya ambayo yalitangazwa mwezi uliopita yamashinikiza vikosi vya Nato kukomesha kuhamisha wafungwa hadi jela kadhaa.
Ripoti hiyo ilifuatia mahojiano yaliyofanyiwa mahabusu 379 wanaoshikiliwa ndani ya jela zinazosimamiwa na idara za kijasusi za Afghanistan, pamoja na polisi nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti hio wengi wao wameonyesha kovu ambazo zimedhihirisha kua aidha walipigwa au kunyanyaswa.
Idara ya kijasusi pia inakabiliwa na tuhuma za mtindo wa kuchagua nani na jinsi gani ya kumnyanyasa mfungwa ili kumshinikiza akiri kua na uhusiano na makundi ya Taliban au kundi lolote la wakereketwa.
Watoto wenye umri wa miaka 14 ni miongoni mwa watu wanaoshikiliwa na waliofikwa na mateso ya aina hio.
Shirika la NATO kwa sasa limesimamisha mpangho wa kuhamisha wafungwa kwa takriban jela 16 nchini humo wakati hali nzima ikifanyiwa uchunguzi.
Serikali haijajibu madai bado haijatoa tamko lolote ingawa mwezxi uliopita ilikanusha madai kama haya ikiyaelezea kama chuki za kisiasa.
0 Comments