MUHEE,MGOGO NA MZARAMO.
Baada ya Mnyamwezi mie juzi kufungwa na katimu kadogo ka Manchester City kwa vijigoli 6 basi Watani wangu wameandamana kwanini sikutoa matokeo ya mchezo huo,WAHEHE wakataka kujinyonga kule Iringa na pale kanda ya kati Dodoma Watani zangu WAGOGO nao wakagoma kabisa kulima Zabibu,kivumbi pale Dar kwa watani zangu WAZARAMOOOO jamaniiii...yani nimeletewa MDUNDIKO nyumbani.
Watani zangu hivi mimi kufungwa kwangu ndio sherehe kwenu? mbona hamkufanya sherehe nilipompa zawadi Arsenal kwa goli 8 au mmesahau? na ile timu ya blue blue Chelsea nilipoipa kipigo cha goli 2 au hamkuona? mashabiki wa Liverpool najua walishukuru MUNGU kwa droo siku ile maana walijua yaleyale ya Arsenal.Sasa nimewawekea picha za magoli na matokeo jinsi tulivyofungwa haya wa Iringa Msijinyonge na nyie wa Dodoma Mkalime Zabibu na nyie watani wangu wa Mdundiko na wapenzi wa Togwa mkacheze bao vizuri(wazaramo). ahsanteni sana nashukuru tunapo pamoja watani wangu popote mlipo Duniani.Mtani wangu wa Sweden tutafutane tusitupane mtani.
Maganga One - Mfalme wa Wanyamwezi.
0 Comments