Mtu mmoja nchini Uganda amehukumiwa kwenda jela kwa miaka 30 kwa mauaji ya mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja, David Kato, mwezi Januari.
Sydney Nsubuga Enoch alikiri kuwa alimponda kichwani na nyundo Bw Kato hadi kufa kwa kutumia nyundo.Amesema shambulio hilo lilitokana na sababu za kimapenzi.
Mauaji hayo yalishutumiwa duniani kote. Waandishi wa habari wanasema tukio hilo lilionesha jinsi unyanyapaa wa wapenzi wa jinsia moja ulivyo nchini Uganda.
Tukio hilo lilitokea wakati bunge la nchi hiyo likijadili kuweka adhabu ya kifo kwa wapenzi wa jinsia moja, kufuatia gazeti moja kuchapisha majina na anuani za wapenzi hao na kuandika kichwa cha habari kisemacho "Wanyongeni hawa".
0 Comments