CHALE 21 alizochanjwa mwanamuziki wa kizazi kipya Bongo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ zimewapa mshtuko watu wake wa karibu na kuanza kuzitafsiri katika matumizi mbalimbali, Ijumaa ‘Kubwa’ linashuka kikamilifu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu ilitokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo washikaji wa nyota huyo walimbaini jamaa ana chale mgongoni zisizopungua 21 katika maeneo mawili.

Chanzo kikadai kwamba, Diamond alichanjwa chale hizo na mganga mmoja maarufu wa mjini Bagamoyo Mkoani Pwani ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

NI CHALE ZA NINI?
Chanzo kikaanika kweupe kuwa chale hizo ndizo zinazomsaidia msanii huyo kung’ara kwa kila wimbo anaoutunga na kuupeleka kwa mashabiki wake na pia kuwa na mvuto kwa mademu ambapo wanamshobokea (wanampapatikia).

“Unajua wenzake wanasema zile chale zinamsadia jamaa kwenye nyimbo zake kuwa bora, lakini pia zinamfanya apendwe na mademu, we si unaona mwenyewe?” kilisema chanzo.

KUHUSU NYIMBO ZAKE
Mpaka sasa Diamond ameshaipua albamu moja ya Mbagala ambayo ina nyimbo vigongo kama Mbagala, Nenda Kamwambie na Moyo Wangu.

MADEMU JE?
Diamond ameshadaiwa kuwa na uhuasiano wa kimapenzi na mastaa na wasio mastaa watano Bongo ambapo amewahi kukiri na kukataa.Mastaa hao ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2008), Jacqueline Wolper (msanii wa filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha Plus), Natasha (msanii wa nyimbo za Bongo Fleva) na sasa Wema Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006 ambaye amevishwa pete ya uchumba miezi miwili iliyopita.



Pendo aliwahi kukaririwa na gazeti moja la Global Publishers akimtaka Wolper aachane na Diamond kwa sababu ni mtu wake.
Hata hivyo, Wolper alikanusha kuwa na uhusiano na msanii huyo akisema hajawahi kutoka naye na kuonya watu kumzushia ingawa kulikuwepo na ushahidi wa kimazingira na mahali walipokutania wawili hao.

Pendo alitoa shutuma hizo baada ya kusoma kwenye gazeti kuwa, Diamond na Wolper wanadaiwa kuwa wapenzi. Wakati huo kasi ya Diomond kuwa staa wa nyimbo za Bongo Fleva ikipamba moto.

Rehema pia mara kadhaa amewahi kuanika uhusiano wake na msanii huyo akidai yeye ndiye wa kwanza, wengine wamedandia kwa mbele.

Natasha yeye aliwahi kuweka wazi kwamba anamfahamu vizuri Diamond na pia anampenda sana bila kufafanua zaidi.

KAULI KUTOKA KINYWA CHA DIAMOND
Sheria ya uandishi inakataza kuchapisha habari ambayo mhusika hajapewa nafasi ya kuzungumza, hivyo Ijumaa lilimtafuta Diamond, lilipompata lilimsomea madai yote kisha likampa nafasi ya kufafanua.

Diamond: Si kweli bwana, chale kweli ninazo ila sababu siyo eti nyimbo zangu zing’are au mademu wanishobokee.
Ijumaa: Sasa ukweli ni upi?Diamond: Nilipokuwa mtoto niliwahi kusumbuliwa sana na ugonjwa wa kichomi cha mara kwa mara, ikafika wakati nikapelekwa kwa tabibu wa tiba asilia ndiyo nikachanjwa chale. Kwahiyo nimekua nazo.

“Kama ni kuhusu nyimbo zangu kufanya vizuri, binadamu lazima waseme kila penye mafanikio. Kama kazi nzuri kwanini isikubalike. Pia mimi sishobokewi na mademu, nakutana nao kama wanavyokutana na wengine.