LILE bifu lililoripotiwa hivi karibuni kati ya mama na mwana ambao ni Wasanii wa Filamu Bongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ na Husna Poshi ‘Dotnata’ limechukua sura mpya baada ya hivi karibuni gazeti hili kunasa comment (maoni) kwenye ukurasa wa Facebook wa Amanda zikionesha kumpiga vijembe mama yake huyo.

Akizungumza na paparazi wa Amani hivi karibuni, mmoja wa watu ambao walikuwa wa kwanza kuziona comment hizo alisema  anashangazwa na hatua aliyofikia Amanda kuhamishia bifu lake kwenye Facebook kwani anahisi litafika pabaya.

“Unajua kwenye Facebook kuna watu wenye akili tofauti unaweza kuandika kitu halafu mwingine akapatia nafasi ya kumtukana huyo uliyemkusudia mwisho mnaanza kushikana mashati huku mwenzenu akiwa amekaa pembeni, mi namshauri Amanda aachane na hayo mambo,” alisema mtu huyo.

Amani liliingia ndani ya ukurasa wa Amanda na kukuta baadhi ya ujumbe wake ukiashiria vijembe hata kama si kwa Dotnata.
Mfano: “Unajua binadamu wapo tofauti, ila siku zote mtu aliyeolewa na dady (baba) wako ni mama yako, sasa akikugeuka huyo anakuwa kituko kidogo.

Hivi inawezekana vipi ukawa na rafiki na adui wa mwanao?”
Ujumbe huu uliandikwa Novemba 4, mwaka huu saa 1: 12 usiku.

Katika toleo la Gazeti la Ijumaa la Novemba 4, mwaka huu, ukurasa wa 16 kulikuwa na habari yenye kichwa; Dotnata, Amanda… BIFU LA AIBU. Inadaiwa