Mwendesha Mashtaka mkuu wa Mahakama ya Uhalifu wa kivita ya ICC ametuma maombi ya kukamatwa kwa Waziri wa Ulinzi wa Sudan kwa tuhuma za uhalifu Darfur.
Luis Moreno-Ocampo alisema Abdelrahim Mohamed Hussein anatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhisi ya ubinadamu uliofanyika mwaka 2003-04
Wakati huo, Bw Hussein alikuwa wakilishi wa Sudan katika eneo lake la magharibi.
Mahakama hiyo yenye makao yake makuu The Hague tayari ilishamshtaki Rais wa Sudan Omar al-Bashir kwa mauaji ya kimbari Darfur
Ombi hilo lilitolewa na ofisi ya Bw Moreno-Ocampo katika taarifa rasmi Ijumaa.
Imeitaka ICC "kutoa hati ya kumkamata waziri wa sasa wa Ulinzi wa Sudan Abdelrahim Mohamed Hussein kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanyika Darfur kuanzia August 2003 mpaka 2004".
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bw Hussein alikuwa ni mmoja wa watu amboa "waliwajibika na uhalifu kwa kiwango kikubwa " kwa mateso makubwa ya Darfur.
Bw Hussein wakati huo alikuwa waziri wa mambo ya ndani wa Sudan.
0 Comments