Wapenzi na wasomaji wa Maganga One Blog,mwaka 2011 leo tukijaaliwa afya njema ndio tunafunga ukurasa na kama kesho tukiamka salama basi tuna ukurasa mpya wa mwaka mpya 2012.Mwaka huu umekuwa ni mwaka wa historia ya kipekee kutokana na matukio tofautitofauti.
Tumeona mengi mazuri yakifanywa na viongozi wetu,tumeona mambo mengi yaliyoongezea maendeleo nchi yetu,japo kuna mapungufu ambayo baadhi yalionekana kwa macho na mengine kusikia kwa masikio na hii yote ni upungufu wa mwanadamu.
Mwaka 2011 ni mwaka wenye matukio mengi makubwa ambayo kwa upande wangu kuna baadhi ya matukio siwezi kuyasahau kirahisi.Mwaka huu tumesheherekea sikukuu ya miaka 50 ya uhuru wetu.
Mwaka huu kumetokea mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kutokea ndani ya nchi yetu, yenye watu wakarimu na upole duniani.
Tukio ambalo naweza kusema lilikuwa kubwa sana kwa upande wangu na kulisahau kirahisi ni vigumu,ni kuondokewa na mama yangu mzazi ambaye alifariki mapema mwa mwezi februari mwaka huu.si rahisi kuelezea ni kiasi gani mshtuko au pigo lililonipata kwa wakati huo.ninachoweza kusema ni kwamba namshukuru Mungu kwa kila jambo.
Mwaka 2011 nimefanikiwa kuongeza wasomaji wengi kwenye blog kulianganisha na siku za nyuma na hii inanipa moyo zaidi wa kuwaletea habari zaidi na zaidi kila kukicha.Pongezi nyingi kutoka kwa wasomaji wengi nimekuwa nikizipokea kwa kuona umuhimu na ubora wa kazi ninazozifanya kila mara kwenye Blog yenu ya Maganga One.
Kadharika kuna baadhi ya watu wachache ambao wamekuwa wakituma maoni ambayo sio mazuri kusomeka kwa jamii kutokana na lugha ngumu walizokuwa wakitumia kuwasilisha ujumbe wao.Kuna maoni mazuri ambayo nimekuwa nikiyapata kutokana na wasomaji wangu nini wanataka niwafanyie na nini hawataki kwenye blog.
Kwa furaha zangu toka moyoni naweza kusema kwamba mwaka huu nimefurahi sana kuwa na wasomaji wangu bega kwa bega ili kuweka sawa mambo kwenye blog yetu.nitafurahi endapo wasomaji wangu mtajihisi huru kunitumia maoni yetu tena kuhusu nini kifanyike kwenye blog yetu ili kuleta maendeleo mazuri kwa wasomaji.
Namtakia kila mmoja sikukuu njema na tuukaribishe mwaka 2012 vyema.Kwa wale wasomaji wapya wajihisi nao ni wamoja kwenye Maganga One Blog.mwenye maoni,ushauri na mengineyo jihisi kuwa huru na mimi kwa kuniandikia ujumbe kupitia magangaone@gmail.com au unaweza kunipigia simu kwa na +32 492 22 33 25 link yetu ni http://magangaone.blogspot.com natumaini kwamba kila mmoja atasheherekea vizuri sikukuu ya mwaka mpya.Ahsanteni sana.
``Maganga One Blogger``.
0 Comments