Klabu ya Asante Kotoko kutoka Ghana.
Klabu ya Manchester United ya Uingereza.
Timu ya Taifa ya Tanzania ( Taifa Stars)
TAFAKURI YANGU:TIMU YA USHINDI HAIANZII UWANJANI
Ama kwa kawaida ni jambo lililozoeleka kuona timu yetu ya taifa ya mpira wa miguu kutofika mbali katika mashindano yeyote pamoja na jitihada zetu kubwa za mashabiki na hata raisi wetu katika kutoa sapoti za hali na mali katika timu yetu.Mimi kama mkereketwa wa taifa langu,
huwa naona uchungu kuona timu yetu inafanya vibaya kila siku na kutoona marekebisho yeyote yanayofanywa na wataalamu ili kurekebisha hali hii.kwa vile mimi si mtaalamu itaniwia vigumu kutaja sababu za kitaalamu hata kama nina ufahamu nazo kidogo juu ya kushindwa kwa timu yetu ya taifa.
Kuna kitu kimoja nimekiona wakati naangalia picha za wachezaji wa timu yetu ya taifa na wachezaji wa timu nje wakati wanaposafiri au wanapowasili kutoka nje kwa kweli kimenigusa, na mimi ninaweza kutoa maoni yangu hapo juu ya kuwa kwa nini tunashindwa katika mchezo wa soka kama mshabiki asiyekuwa mtaalamu katika masuala ya ufundi wa soka.
Kwa kawaida wasifu(muonekano) wa nje mara nyingi huakisi wasifu wa ndani kwa asilimia hamsini na hata zaidi ya hapo katika kitu chochote.Tukiangalia wachezaji wetu wanavyovaa kwa kweli utawaona hawavai kitimu hata wanapotembea wanapokua pamoja bado utaona kila mtu yuko kivyake vyake je kwa stahili hii tutashinda kweli kwa kutegemea kuingia uwanjani na kucheza tu? Kwa sababu kama vipaji naamini wachezaji wetu wanavyo lakini ukweli ni kwamba maandalizi ya timu yeyote huanzia nje ya uwanja yaani mikakati na mojawapo niwachezaji kuwa kitu kimoja ili wapate kuwa na morali wa kufanya vizuri kwenye mashindano na mojawapo ya wachezaji kuwa kitu kimoja ni kuvaa sare nadhifu zitazowatambulisha wao juu ya utaifa wao na wao kujiona watu(proud) mbele ya mashabiki wao wa nyumbani na hata wale wa upinzani na pia kutembea kama timu mbele za watu.
Kama tukiangalia picha hapo juu nadhani inajitosheleza ni jinsi gani tusivyo makini katika masuala yetu.Najaribu kujiuliza na hili ni kosa la nani?je ni kwamba hatuna wadhamini wanaoweza kutustiri kisare juu na chini?Au wachezaji wetu wenyewe ni wasela mno kiasi cha kwamba hawapendi sare na hata hizo fulana wamevaa kana kwamba hakuna jinsi watafanyaje?Na je sisi washabiki tunaowaona wachezaji wawenzetu wako nadhifu na wenye muonekano wakujiamini wanapoingia katika ardhi ya nchi yetu tunafikiriaje?kwa mimi binafsi ninaweza kuvutiwa nao na uzalendo ukanitoka.
Na hii ni tafakuri yangu ya leo.
Shekh Hija-Den Haag,Holland.
Maganga One nasema mwenye maoni Ruksaaa!!!
0 Comments