Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Dec 10, 2011

WEMA SEPETU KUTOA KITABU CHA MAISHA YAKE NA WANAUME WOOTE ALIOJIMWAYAMWAYA NAO,ASEMA AMEWATAJA WOTE KWA MAJINA MPAKA WAUME ZA WATU NDANI

MISS Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu, ametaja wanaume alioduu nao tangu aliposhiriki mapenzi kwa mara ya kwanza hadi sasa.

Orodha ya wanaume walioduu na staa huyo wa filamu kwa sasa, ipo kwa ukamilifu wake kwenye kitabu cha Wema ambacho kinazungumzia maisha yake.

Wema ameamua kutoa kitabu kinachozungumzia historia ya maisha yake ili kuwafanya watu wanaotaka kumjua kwa undani, wasome na kujionea kile ambacho hakijaonwa popote.

Katika kufanikisha kitabu hicho, Wema ameingia mkataba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo ambaye amekubali kukisimamia mwanzo hadi mwisho kitakapoingia mitaani.
 
Shigongo alipozungumza na gazeti hili, alikiri kufanya makubaliano na Wema kwa ajili ya kutoa kitabu hicho na kueleza kwamba ni jambo zuri.

“Mtu kutoa kitabu kinachohusu maisha yake ni uamuzi wa busara. Kitabu ndicho kinachoweza kumfanya Wema aendelee kubaki kwenye historia ya nchi kwa miaka mingi ijayo hususan kwa wapenzi wa burudani.“Lilipokuja wazo hili la kutoa kitabu, kwangu mimi sikuwa na ajizi ya kumpa sapoti Wema aweze kuandika kitabu cha maisha yake, nafikiri watu wengi ambao wana kiu ya kumjua kwa undani, watapata fursa hiyo kupitia kitabu chake,” alisema Shigongo.

Wema alipoulizwa kuhusu kitabu hicho, alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa sababu anatambua anao mashabiki wengi ambao wanapenda kumsoma na kumjua kwa undani zaidi.
 
“Ndani ya kitabu hicho, kuna idadi ya wanaume ambao nimekuwa na uhusiano kuanzia mtu wa kwanza mpaka wa mwisho,” alisema Wema. “Nimewataja na majina kabisa, sijamuacha mtu.”

Kuhusu kutaja majina ya wanaume alioduu nao, Wema alikiri kuwa inaweza kuzua hofu kwa sababu wengine ni waume za watu lakini akasisitiza kuwa atakuwa mkweli kwa asilimia 100.

“Ni safari ya maisha yangu. Nataja kila kitu kwa sababu nataka kila hatua ya maisha yangu iwe kwenye kitabu.
Hivyo, siwezi kuacha kutaja jina kwa sababu ni mume wa mtu au vinginevyo,” alisema Wema.
 
Mchumba wa Wema, Abdul Naseeb ‘Diamond’ alipoulizwa kuhusu uamuzi wa mkewe mtarajiwa alisema haina shida.
“Mimi sioni shida, najua kila kitu na nimembariki, watu wakae mkao wa kukisoma kwani kinavutia,” alisema Diamond.Wema ameamua kutoa kitabu kinachozungumzia historia ya maisha yake ili kuwafanya watu wanaotaka kumjua kwa undani, wasome na kujionea kile ambacho hakijaonwa popote.

Katika kufanikisha kitabu hicho, Wema ameingia mkataba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo ambaye amekubali kukisimamia mwanzo hadi mwisho kitakapoingia mitaani.
 Shigongo alipozungumza na gazeti hili, alikiri kufanya makubaliano na Wema kwa ajili ya kutoa kitabu hicho na kueleza kwamba ni jambo zuri.

“Mtu kutoa kitabu kinachohusu maisha yake ni uamuzi wa busara. Kitabu ndicho kinachoweza kumfanya Wema aendelee kubaki kwenye historia ya nchi kwa miaka mingi ijayo hususan kwa wapenzi wa burudani.

“Lilipokuja wazo hili la kutoa kitabu, kwangu mimi sikuwa na ajizi ya kumpa sapoti Wema aweze kuandika kitabu cha maisha yake, nafikiri watu wengi ambao wana kiu ya kumjua kwa undani, watapata fursa hiyo kupitia kitabu chake,” alisema Shigongo.

Wema alipoulizwa kuhusu kitabu hicho, alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa sababu anatambua anao mashabiki wengi ambao wanapenda kumsoma na kumjua kwa undani zaidi.
“Ndani ya kitabu hicho, kuna idadi ya wanaume ambao nimekuwa na uhusiano kuanzia mtu wa kwanza mpaka wa mwisho,” alisema Wema. “Nimewataja na majina kabisa, sijamuacha mtu.”

Kuhusu kutaja majina ya wanaume alioduu nao, Wema alikiri kuwa inaweza kuzua hofu kwa sababu wengine ni waume za watu lakini akasisitiza kuwa atakuwa mkweli kwa asilimia 100.

“Ni safari ya maisha yangu. Nataja kila kitu kwa sababu nataka kila hatua ya maisha yangu iwe kwenye kitabu.
Hivyo, siwezi kuacha kutaja jina kwa sababu ni mume wa mtu au vinginevyo,” alisema Wema.
Mchumba wa Wema, Abdul Naseeb ‘Diamond’ alipoulizwa kuhusu uamuzi wa mkewe mtarajiwa alisema haina shida.
“Mimi sioni shida, najua kila kitu na nimembariki, watu wakae mkao wa kukisoma kwani kinavutia,” alisema Diamond. 
 
Share this article :

0 Maoni:

Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP