Afisa misaada mwandamizi nchini Uingereza amefukuzwa nchini Chad wakati alipojaribu kutembelea kambi ya wakimbizi ambao bado wanaishi mashariki mwa nchi.
Mukesh Kapila alikuwa mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan aliyezungumza wazi wakati mgogoro wa Darfur ulipoanza miaka tisa iliyopita.
Waziri wa mambo ya ndani wa Chad binafsi ameamuru afisa huyo kuondoka nchini.
Bw Kapila anasema sababu za kufukuzwa kwake kunahusiana na ushirikiano wa karibu uliopo kati ya serikali ya Sudan na Chad ambao amewatuhumu kuhusika na mauaji ya kimbari.
Hii ilikuwa ni ziara ya kwanza ya Bw Kapila kuzuru eneo hilo tangu alipoondolewa katika nafasi yake mwaka 2004 akiwa amechanganyikiwa na kushindwa kuwashawishi jumuiya kimataifa kuchukua hatua kwa hali iliyokuwepo wakati huo Darfur, aliamua kuzungumza kwa umma alipozungumza na
BBC.
Bw Kapila anatishiwa na kivuli chake mwenyewe baada ya kushindwa kuzuia mauaji Darfur.
Kiasi cha watu milioni 2.7 wameyakimbia makazi yao tangu mgogoro uanze katika eneo hilo la magharibi lenye ukame. Na Umoja wa Mataifa unasema karibu watu laki tatu wamekufa kutokana na vita, njaa na magonjwa.

Kufukuzwa kisiasa?

Bw Kapila alikuwa kutembelea makambi ya wakimbizi mashariki mwa nchi ambako watu 200,000 bado wanaishi."nilichanganyikiwa, nimehuzunishwa sana na kukasirishwa mno," aliiambia BBC alipojua kuwa amefukuzwa nchini humo.
Bw Kapila anaamini kuwa sababu ya kufukuzwa kwake inahusiana na kuwepo kwa ushirikiano kati ya N'Djamena na Khartoum.