Msemo wa zamani kwamba ``Vijana ndio Taifa la kesho``,kwa mtaji huu waungwana tutegemee nini hapa?hali hii inatisha,kusikitisha na kukatisha tamaa kabisaa.sina maana mbaya kwa wahusika ila bila jitihada binafsi taifa litaendelea kuwa masikini mpaka dunia inakwisha.viongozi wetu muwe na uchungu wa ukweli mnapotaka madaraka ili kuwatumikia wananchi.wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,wabunge msitegemee kila kitu atafanya rais,nyie ndio viongozi wa karibu sana na wananchi wenu na mnaziona shida zao kwa ukaribu sana,Msisubiri mpaka kipindi cha uchaguzi ili mpite kila nyumba kuomba kura wakati matatizo kama hayo pichani yanawezekana kabisa kuyasawazisha.Huu ni ujumbe wangu kwenu ila msinihukumu kwani najua ukweli siku zote unauma.
0 Comments