Waziri wa zamani wa habari wa serikali ya Gambia amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kupanga kupanga mapinduzi ya kumowndoa Yahya Jammeh.
Amadou Scatred Janneh – ambaye pia ni raia wa Marekani alikutwa na hatia ya kutaka kufanya mapinduiz na kusambaza fulana zenye uchochezi.
Wengine watatu wamehukumiwa miaka sita jela na kazi ngumu.
Rais Jammeh – aliyeingia madarakani katika nchi hiyo ndogo ya Afrika Magharibi katika mapinduzi ya umwagaji damu mwingi mwaka 1994 – anatuhumiwa kwa kuwakandamizi wakosoaji wake.
Bw Janneh, mwenye miaka 48, alikuwa waziri wa mawasiliano mwaka 2005 na 2006.
Aliwahi kuwa afisa mwanasiasa na mchumi katika ubalozi wa Marekani mjini Banjul, mji mkuu wa Gambia – kituo maarufu kwa watalii kutoka Ulaya.
Fulana za watuhumiwa wengine wanne walituhumiwa kwa kusambaza mwaka jana zenye maneno "mmungano wa mabadiliko Gambia , Maliza udikteta sasa".
Mawakili wa Bw Janneh wanasema watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, shirika la AFP linaripoti.
Rais Jammeh alichaguliwa tena mwezi Disemba kwa awamu ya nne ulishutumiwa na kususiwa na waangalizi wa kimataifa.