Mtoto huyu mdogo aliyenaswa na mpiga picha wetu akiomba pesa kwa wapita njia,hii desturi inazidi kukomaa katika bara letu la Afrika.sio kwamba watoto hawa hawana wazazi au wana maisha magumu hivyo ila ni desturi za wazazi kuikubali hali hiyo pindi wakiletewa pesa na watoto wao nyakati za jioni,picha hii imenaswa mpakani mwa Uganda na Kenya sehemu inayoitwa Busia.(Picha na Daniel wa Maganga One Blog).
Ukiangaliza picha hii nayo unaweza kumuona mwanaume aliyetimiza viungo vyote na nguvu zake ila amekaa kitako na kijikopo akiomba pesa kwa wapita njia huku akiwa na simu mkononi.Viongozi husika angalieni sana wananchi wenye kasumba kama hizi ni kuwaondosha mitaani kwani wanalitia aibu taifa.hapo ni Busia mpakani mwa Uganda na Kenya.
Ona na haka katoto masikini ya MUNGU kamewekwa nako ili wasamaria wema wakaonee huruma,hii ni staili ya wazazi jinsi ya kuomba pesa.hapa ni ndani ya jiji la Kampala nchini Uganda.
Tukiwa bado ndani ya jiji la Kampala nchini Uganda kamera yetu ya Black Berry iliendelea kuwanasa watu wenye uwezo wa kufanya kazi ila wapo mitaani wakiombaomba.mama kama huyo pichani hivi akijishughulisha kulima mbogamboga na kuuza sokoni kuna tatizo?
Kwa mtaji huu tutegemee nini kwa taifa la kesho?mtoto aliyepaswa kuanza shule ya vidudu hapo anaanza kuombaomba.miji mikubwa Afrika utia aibu kwa watalii kuona hali kama hii,hapa ni Kampala nchini uganda.(Picha zote na Daniel wa Maganga One Blog,Kampala).
0 Comments