Majaji nchini Italia wamemuweka nahodha wa meli ya kifahari, ijulikanayo kama Costa Concordia, iliyopinduka katika ufuo wa bahari nchini humo siku ya Ijumaa iliyopita, chini ya kizuizi cha nyumbani.
Waendesha mashtaka wanasema Francesco Schettino, alisababisha ajali ambayo ilipelekea meli hiyo kupinduka na kwamba aliondoka kutoka kwa meli hiyo kabla ya abira wote walikuwa ndani yake kuokolewa.Sauti zilizorekodiwa za mazungumzo kati ya Schettino na afisa mmoja wa bandari baada ya ajali hiyo inaonekana kuunga mkono madai hayo, ingawa nahodha huyo amekanusha madai hayo.
Katika mazungumzi hayo yaliyorekodiwa, yaliyochapishwa na gazeti la Italia la Corriere della Sera, afisa huyo wa bandari, Gregorio de Falco anasikika akimwambia Schettino mara kadhaa arudi kwa meli hiyo kuwasaidia abiria waliokwama.
"Schettino, pengine ulijiokoa mwenyewe kutoka baharini , lakini nitahakikisha kuwa umewajibika. Rudi kwenye meli yako," afisa huyo wa bandari alinukuliwa akisema.
Schettino pia amelaumiwa na mwenye meli kwa kuacha makusudi kufuata njia ya kawaida ya meli hiyo.
Hata hivyo nahodha huyo anasisitiza kuwa alifuata utaratibu sawa wakati wote alipokuwa katika meli hiyo.
Kufikia sasa abiria 20 hawajulikani walipo.
Miongoni mwao ni raia wa Ujerumani, Italia, Ufaransa na Marekani.
0 Comments