Pichani juu: Chalz Baba akiwa na Wema enzi za penzi lao, picha nyingine Wema akiwa amepozi nyumbani kwake na inayofuata ni sebule ya nyumba yake.
Na Shakoor Jongo
MWANAMUZIKI gumzo kwa sasa aliyechomoka katika Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta International’ na kusaini mkataba kwenye Bendi ya Mashujaa kwa ada ya Sh. milioni 15, Charles Gabriel ‘Charlz Baba’, amesogea mtaa anaoishi Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Charlz Baba ametumia jeuri ya mamilioni hayo ya Mashujaa, kusaka nyumba kwa gharama yoyote jirani na anapoishi Wema aliyewahi kuwa mpenzi wake maeneo ya Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Habari za uhakika zilisema kuwa, Charlz Baba amehamia mtaani hapo mita chache kutoka nyumba anayoishi Wema mara baada ya kurejea kutoka Dubai alipokwenda kwa mapumziko mafupi.
Ilidaiwa kuwa dau hilo alilolamba limempa jeuri ya kuyaacha maskani yake ya zamani maeneo ya Block 41 Kinondoni, Dar alipokuwa amepangisha kwa muda mrefu.
Ilibumburuka kuwa, Charlz Baba aliyetambulishwa rasmi kwenye Bendi ya Mashujaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Business Park Kijitonyama, Dar, amechukua nyumba nzima yenye vyumba kadhaa vya kulala, sebule, jiko na bafu ikidaiwa kuwa amelenga kumnasa Wema kimapenzi.
 RISASI MZIGONI
Baada ya kumwagiwa ‘upupu’ huo

, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Charlz Baba ili kupata undani wa taarifa hizo ambapo alikiri kuhamia mtaani hapo.
Alipoulizwa kama ni kweli alihamia eneo hilo ili kumrudisha Wema kwenye himaya yake kimapenzi alisema:
“Mwanzoni sikujua kama Wema alikuwa anaishi mtaa ule, ila nilipoambiwa na madalali kwamba yuko maeneo hayo, nilihakikisha napata nyumba.
“Nilitamani sana kuwa jirani yake. Huwa nafarijika sana kuwa karibu naye, naamini siku moja moja tutakuwa tunatembeleana.”

WEMA KIZIMBANI
Wema alipoulizwa na paparazi wetu kama ana habari kuwa anaishi mtaa mmoja na Charlz Baba, alishtuka na kusema:
“Acha bwana…anakaa nyumba gani? Hebu nielekeze. Ni kweli anaishi mtaa huu?”
Alipoelekezwa hadi mlango wa nyumba anayoishi Charlz Baba mtaani hapo, Wema aliangua kicheko: “Teh…teh...teh.”
Alipoambiwa kuwa jamaa huyo amehamia mtaani hapo ili kurejesha penzi lao kama zamani, Wema aliahidi kumpigia simu mwandishi wetu baadaye ili kulizungumzia hilo.
Hata hivyo, hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, Wema hakupiga simu na hata alipopigiwa simu yake iliita bila kupokelewa.
Wema na Charlz Baba waliwahi kuwa na mapenzi ya njiwa kabla ya Bwa’mdogo wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ kuchukua mtoto.